Wakizungumza kwajazba kwenye mkutano ulioitishwa na kamati ya
ulinzi na usalama ya wilaya ya Morogoro kwa lengo la kujadili chanzo cha
vurugu zilizosababisha mwenyekiti huyo kupigwa na wananchi wake mnamo
Januari 15 mwaka huu wakiwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji wananchi hao
wamesema hawawezi kuvumilia viongozi wasio waadilifu wanaosababisha
migogoro kati ya wakulima na wafugaji na kutaka kamati hiyo iondoke naye
vinginevyo wata mshughulikia kwa kumshushia kipigo.
Pamoja na katibu tawala wa wilaya ya Morogoro Bwana Alfredi Shayo
kujaribu kusuluhisha mgogoro huo kwa kuwashauri wananchi hao kufuata
taratibu za kumuondoa mwenyekiti huyo kwa kuitisha mkutano mkuu wa
kijiji lakini jitihada hizo zimegonga mwamba jambo ambalo limezua mzozo
mkubwa baina ya kamati hiyo na wananchi na mambo yakawa hivi.
Baada ya hali ya usalama wa mwenyekiti Ismail kuwa tete huku
wananchi wakizingira magari ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya
mwenyekiti huyo ameamua kujitokeza na kutangaza kijiuzulu wadhifa wake
na hapa anasema.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini