wanajeshi kamisheni Monduli mkoani Arusha watunikiwa. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Saturday, January 23, 2016

wanajeshi kamisheni Monduli mkoani Arusha watunikiwa.

Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Mh rais Dr John Pombe Magufuli ametunuku kamisheni kwa maafisa wanafunzi 205 kutoka ndani na nje ya nchi wa cheo cha Luten USU waliohitimu mafunzo katika chuo cha mafunzo ya kijeshi cha (TMA) kilichoko Monduli mkoani Arusha.
kabla ya Mh rais kutunuku kamisheni hizo alikagua Gwaride na kutoa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri darasani na pia kwenye medani akiwemo mwanafunzi mwanamke kutoka Kenya.
 
Baada ya Mh rais kutunuku kamishen kwa maafisa hao ambao 10 wanatoka nchi rafiki ikiwemo Kenya na Burundi na 16 kati ya wote wakiwa ni wanawake walikula kiapo cha utii kwa Mh rais.
 
Katika sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi na watendaji mbalimbali wa serikali wakiwemo waziri wa ulinzi Dr Husein Mwinyi mkuu wa majeshi Generali Davis Mwamunyange na mkuu wa majeshi mstaafu General Mrisho Sarakikya.
 
Wengine ni pamoja na katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Felexs Ntebenda wakuu wa wilaya za mkoa wa Arusha wawakilishi kutoka nchi jirani na wanachi.
 
Shereh hizo zilipambwa na burudani ya vikundi vya ngoma kikiwemo cha jeshi la kujenga taifa kambi ya Oljoro.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin