Wakuu wa shule za sekondari Mwanza wavuliwa madaraka kwa tuhuma za ubadhirifu. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Friday, January 29, 2016

Wakuu wa shule za sekondari Mwanza wavuliwa madaraka kwa tuhuma za ubadhirifu.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo amevunja bodi ya shule ya sekondari Pamba iliyopo jijini Mwanza na kumvua madaraka mkuu wa shule hiyo Aidan Dotopery pamoja na walimu wengine wawili kutokana na kushindwa kusimamia vyema matumizi ya fedha na mali za shule zao.
Walimu wengine waliovuliwa nyadhifa zao na mkuu huyo wa mkoa ni pamoja na mkuu wa shule ya sekondari Nyakurunduma January Luganyika na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyamagana Masau Mtakilolwa.
 
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza kufanya ziara katika shule hizo na kuonyesha kutoridhishwa na mazingira ya uwekezaji kwenye vitega uchumi vya shule ya sekondari ya Pamba, huku baadhi ya nyaraka pamoja na mikataba ambayo shule hiyo imefunga na wafanyabiashara hao ikiwa imegubikwa na utata.
 
Mwalimu January Ruganyika ambaye aliwahi kuwa mkuu wa shule ya sekondari Pamba kabla ya kuhamishiwa sekondari ya Nyakurunduma, ameshushwa madaraka yake baada ya kugundulika kuwa hakuwa makini katika kuhakikisha mali za shule hiyo pamoja na fedha zinatumika kwa manufaa ya shule na sio kukuta mikataba mibovu na yeye kuamua kuiendeleza bila kutafuta ufumbuzi wake.
 
Kwa hali hiyo mkuu huyo wa mkoa amemuagiza mkurugenzi wa jiji la Mwanza kuwapangia vituo vingine vya kazi kama walimu wa kawaida kwa kushindwa kuwajibika katika nyadhifa zao na kutekeleza majukumu yao kikamilifu, huku mkuu wa shule ya sekondari Pamba Aidan Dotopery akilazimika kujenga hoja za utetezi.
 
Lazaro Nyambura, mmoja wa walimu wa shule ya sekondari Pamba ameiomba serikali kuingilia kati sakata hilo katika kutafuta kiini cha tatizo la shule hiyo kwani wahusika walionufaika na miradi hiyo wapo salama salimini lakini wanasababisha mateso kwa walimu wengine ambao wanalazimika kutumikia adhabu isiyo wastahili.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin