LHRC yapinga hatua ya serikali kuzui bunge kurushwa moja kwa moja kwenye TV ya taifa. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Friday, January 29, 2016

LHRC yapinga hatua ya serikali kuzui bunge kurushwa moja kwa moja kwenye TV ya taifa.


Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC, kimepinga hatua ya serikali kuzuia matangazo ya bunge kurushwa moja kwa moja kupitia kituo cha luninga ya taifa, na kwamba hatua hiyo inakwenda kinyume cha sheria na haki ya wananchi ya kupata taarifa uhuru wa kutoa maoni.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa LHRC, Emelda Urio, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam ambapo ameitaka serikali kuheshimu haki ya kupata taarifa na uhuru wa habari kwa kuweka mazingira wezeshi kwa watanzania wote kupata habari na taarifa zinazowahusu kwa wakati ambazo ni wezeshi na zitakazowawezesha kufanya maamuzi sahihi.
 
Aidha kituo hicho kimeitaka serikali kutekeleza kwa vitendo maazimio na makubaliano ya kimatafa ya kikanda katika kulinda haki ya kupata taarifa kwa kufuta sheria kandamizi zenye kuminya uhuru na inapaswa kutenga rasilimali za kutosha kuwezesha matangazo ya moja kwa moja kwa TBC kuhusu mwenendo mzima wa bunge.
 
Kwa upande wake afisa mwandamizi wa LHRC ameutaka uongozi wa bunge kufanya kazi ya kuimarisha mhimili huo kulingana na wadhifa waliopewa na kuweka mazingira wezeshi ya majadiliano na maridhiano na kutokutoa mianya ya kuingiliwa kwa bunge na mihimili mingine
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin