Serikali imesema imeadhimia mwaka wa fedha wa
2016/2017 kushusha kiwango cha tozo la kodi kwa mfanyakazi kutoka
asilimia 11 ya hivi sasa hadi kufikia asilimia 10 kwa mwaka huo wa
fedha.
Naibu Waziri wa Fedha na Mpingo Mhe. Ashantu Kijaji.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mpingo Mhe. Ashatu Kijaji wakati
wa kipindi cha maswali na majibu leo bungeni ambapo amesema kuwa lengo
la serikali ni kushusha zaidi hadi kufikia digiti moja.
Mhe. Ashatu ameongeza kuwa baada ya kufikia asilimia 10 ya tozo la kodi hiyo serikali itakaa na wadau ikiwemo vyama vya wafanyakazi ili kutafuta ufumbuzi wa ni namna gani wanaweza kushusha zaidi kutokana na ukuaji wa uchumi siku hadi siku.
Katika hatua nyingine Mhe Ashatu amesema kuwa serikali imedhamiria kupandikisha kiwango cha pensheni kwa wazee wastaafu hadi kufikia shilingi laki mbili na nusu kadri ya uchumi utakavyoimarika na mikakati tayari imeshaanza kuandaliwa.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini