Serikali
imeuwasilisha na kuuondoa mpango wa pili wa maendeleo ya taifa kwa
kipindi cha miaka mitano baada ya kubainia kuwa kuna kanuni na tararibu
ambazo zimekiukwa katika kuwasilisha mpango huo bungen.
Mpango huo ambao uliwasilishwa bungeni na waziri wa fedha na
mipango Mh Dk Philip Mipango ulibainisha mapendekezo ya mwelekeo wa pili
wa maendeleo kwa miaka mitano ijayo ya serikali kwa kipindi cha miaka.
Baada ya waziri wa fedha kuwasilishwa mpango huo Mh Zitto kabwe na Mh Tundu Lissu walioamba miongozo juu ya jambo hilo.
Hata hivyo mwenyekiti wa bunge Mh Andrew Chenge aliwaambia wabunge
hao kuwa jambo hilo amelichukua anahitaji muda kulifanyia kazi nahivyo
kuruhusu taratibu zingine kuendelea na ulipofika muda wa kambi ya
upinzani kuwasilisha hotuba yao wakagoma.
Kisha Mh Chenge akalazimika kuahirisha bunge kablya ya muda.
Baada ya kuahiriswa kwa kikao hicho na bungeni kurejea jioni ndipo waziri mwenye dhamana alipoamua kuondoa mpango huo bungeni.
Kufuatia hatua hiyo baadhi wabunge hasa wa upinzani akiwemo Mh
James Ole Milya amesema kitendo cha kuondolewa kwa hoja hiyo ni ishara
nzuri kwa serikal i kuwa imeanza kuyafanyia kazi mawazo yao.
ITV ilimtafuta waziri wa katiba na sheria Mh Dk Harrison Mwakyembe
ambaye amesema kilichotoke ni tatizo la kiufundi tuu na jumatatu
litarekebishwa.
Awali waziri wa fedha Mh Dk Philip Mipango aliwasilisha mpango huo
na kubainisha mambo mbalimbali na maendeleo kwa kipindi cha miaka
mitano ijayo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini