Mwili
wa mtu mmoja umeopolewa mto Kilombero mkoani Morogoro katika juhudi
zinazoendelea mpaka sasa za uokozi baada ya kivuko cha MV 2 kuzama juzi.
Kwa mujibu wa mwandishi weyu Sifuni Mshana aliyeko eneo la tukio
mwili huo umeopolewa baada ya juhudi za wananchi wa kawaida waliojitolea
kuzamia kwa ajili ya kusaidia shughuli hiyo ya uokozi.
Hata hivyo kikosi cha jeshi la wanamaji kimefika eneo la tukio na
halijafanikiwa kuokoa mtu yeyote mpaka sasa japo wanaendelea na harakati
hizo.
Idadi ya watu isiyo fahamika mara moja wanahofiwa kufa maji
yakiwemo magari matatu kudumbukia baada ya kivuko cha MV 2 Kilombero
kuzama katikati ya mto Kilombero kufuatia upepo mkali.
Ulioambatana na mvua kubwa kunyesha juzi majira ya saa moja na nusu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini