Rais
wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewaapisha
mawaziri wane ikulu jijini Dar es Salaam huku wakiahidi kuhakikisha
wanasimamia kikamilifu utekelezaji wa sera ya hapa kazi tu.
Katika mahojiano na ITV baada ya kula kiapo mbele ya rais Dkt John
Magufuli, mawaziri hao wamesema wamejipanga kuhakikisha watanzania
wananufaika na rasilimali za nchi.
Kwa muda mrefu wizara ya maliasili na utalii imekuwa na changamoto
kubwa ikiwemo ya kushindwa kusimamia rasilimali asili, lakini huenda
suluhisho limepatikana.
Zoezi hilo la uapisho limeshuhudiwa na makamo wa rais na waziri
mkuu ambapo mawaziri hao ni pamoja na Prof Jumanne Maghembe ambaye ni
waziri wa mali asili na utalii, Dkt Joyce Ndalichako waziri wa elimu
sayansi, teknolojia na ufundi, Dkt Philip Mpango waziri wa fedha na
mipango, Mhandisi Gerson Lwenge waziri wa maji na umwagiliaji na Prof
Makame Mbarawa waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini