umoja wa ulaya
umekaribia kukubaliana juu ya makubaliano ya Schengen katika suala la
kufungua mipaka baina yao kusitishwa mpaka baada ya miaka miwili
kutokana na kufurika kwa wahamiaji na wakimbizi .Katika kikao cha
mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi za ulaya huko Amsterdam kilichoibuka
na mapendekezo kuwa Ugiriki inapaswa kutengwa katika jumuiya ya schengen
kama haitaweza kufuata masharti yaliyowekwa.
Waziri wa uhamiaji
wa Ugiriki,Yiannis Mouzalas alisisitiza kuwa nchi yake inafanya kila
iwezalo ili kutatua tatizo la madeni yanayowasakama.Ugiriki imechoka
kusikia kuwa mipaka yao haitalindwa kwa sababu ya madeni.Umoja wa ulaya inasema ni takribani waamiaji zaidi ya elfu mbili wanaingia Ugiriki kila siku licha ya kwamba kuna bahari na kuna hali ya hewa ya kipupwe kikali
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini