Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewaambia viongozi wa Afrika kwamba
anaunga mkono pendekezo lao la kutuma askari 5,000 wa kuweka amani huko
Burundi.
Alisema hayo katika mkutano wa viongozi wa nchi za AU
nchini Ethiopia, ambako viongozi hao watapiga kura kuunga mkono au
kukataa pendekezo hilo.Rais wa Burundi , Pierre Nkurunziza, amelipinga pendekezo hilo - Burundi inasema kutuma wanajeshi huko itaonekana kama uvamizi.
Uamuzi wa rais huyo kugombea muhula wa tatu wa uongozi ndiyo uliozusha ghasia za miezi kadha.
Kiongozi wa Gambia, Yahya Jammeh, ambaye alinyakua madaraka kwa kupindua serikali, alisema hatounga mkono pendekezo hilo iwapo Burundi haitoridhia.
Na rais wa Chad, Idris Deby, amepokea nafasi ya uenyekiti wa AU kutoka kwa kiongozi wa Zimbabwe, Robert Mugabe.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini