.

Takribani
wafanyabiashara 28 wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya pombe haramu
ya Moshi maarufu kama Gongo katika kijiji cha Barjomod wilayani Hanang
mkoani Manyara wamenusurika kushambuliwa na kubomolewa makazi yao
sambamba na kufukuzwa kijijini hapo na wananchi zaidi ya 500 wenye
hasira baada ya kugundulika kukiuka sheria ndogo ya kijiji na kuendelea
kuuza pombe hiyo iliyosababisha vifo vya watu watano.
ITV ilishuhudia msako huo wa nyumba kwa nyumba, shamba kwa shamba
maeneo yanayoaminika kufanyika na kufichwa kwa pombe hiyo ambayo baadhi
ya wazee wa mila na desturi wamesema imechangia kudhoofisha nguvu kazi
kwa vijana na kushindwa kuoa, familia kutelekezwa, vipigo kwa wanawake,
vifo na kushuka kwa maadili.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho cha Barjomod kilichopo kata
ya Gitting Bw William Basso mbele ya mkutano ulioitishwa na wazee wa
mila anasema msako huo umedumu kwa siku saba usiku na mchana na
wamelazimika kuwatoza wafanyabiashara tozo la Ng’ombe 30 wakiwemo
wenyeviti wa vitongoji walioshindwa kudhibiti biashara hiyo na mifugo
hiyo wamekuwa wakifanya karamu badala ya kuuza.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Hanang Bw Thobias Mwilapwa alipoulizwa
juu ya uhalali wa tozo hilo amesema kulingana na wazee hao wa mila na
desturi wanalenga kukomesha uhalifu kupitia biashara hiyo inayosababisha
vifo amesema lazima wazingatie sheria za nchi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini