Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene amekuwa kiongozi
wa pili kumhoji Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusu mradi
wa mabasi wa Udart. Jana Simbachawene alipotembelea mradi huo alimtaka
Makonda kuweka askari wa kutosha watakaodhibiti uvunjwaji wa sheria
katika mradi huo.
Huyo
ni kiongozi wa pili kumhoji Makonda kuhusu mradi wa Udart, baada ya
hivi karibuni Rais John Magufuli kumtaka asimamie kwa kutoa adhabu kali
kwa wale watakovunja sheria kwenye mradi huo.
Katika
ziara yake jana, Simbachawene alipanda gari nambari T121DGW kutoka
Kimara mpaka Kiarikoo Gerezani na alipofika alipokelewa na Mkuu wa Mkoa,
wakuu walaya na viongozi wengine.
Hata
hivyo, aliwataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa mpya kwa kujenga
vituo vya maegesho ya magari karibu na stendi za mabasi ya haraka ili
watu wanaotaka kwenda mjini wawe wanaegesha magari yao na kupanda mabasi
hayo, ambako mbali na kuwahi kazini wataokoa gharama za mafuta.
Katika hatua nyingine;
Simbachawene amepiga marufuku ombaomba na wafanyabiashara maeneo ya
mjini na kumtaka Makonda kutekeleza maagizo hayo kwa kuweka askari wa
kuwaondoa.
Alisema
watu wanaowapa ombaomba pesa siyo kwamba wana mipango mizuri na
Serikali kwa kuwa watoto wanaotumika kuomba walitakiwa wawe shule.
Makonda alisema kuwa utekelezaji wa maagizo hayo umeanza mara moja, kwani yaliyotolewa yapo kwa mujibu wa sheria.
Hata
hivyo, Makonda alisema kuwa ana mpango wa kuongeza muda wa kufanya
biashara katika maduka makubwa na katika soko la Karikaoo kuwa mpaka saa
nne za usiku.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini