CHAMA
cha wananchi CUF kimesema mkutano mkuu wa taifa ambao unategemewa
kumpata Mwenyekiti wa chama hicho, upo pale pale, na kuweka msimamo
kuhusu Ibrahimu Lipuma kuwa kama anataka kurejea katika nafasi yake
achukue fomu.
Tamko
hilo ni kufuatia sintofahamu kwa wanachama wa chama hicho kuwa huenda
mkutano mkuu usiwepo kutokana na ujio wa ghafla wa Prof. Ibrahim Lipumba
aliyekua Mwenyekiti wa chama ambaye alijihudhuru cheo hicho.
Shaweji
Mketo, Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho amesema tayari fomu za
ugombea zimeshapelekwa katika ofisi ya wilaya tayari kwa kujazwa.
“kuanzia
1 Julai washiriki katika ngazi ya Mbali mbali ikiwemo Mwenyekiti wa
chama pamoja na Makamu mwenyekiti wachama hicho na wataanza kuchukua
fomu hadi Julai 20,” amesema.
Amesema,
21 Agosti baada ya zoezi la ujazaji fomu kukamilika, wajumbe wa Mkutano
Mkuu wa chama hicho Kitaifa watakaa kuchagua viongozi hao katika ukumbi
wa Land Mark Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Lipumba
alijihudhuru katika kipindi cha uchaguzi Mkuu 25 Oktoba kutokana na
sababu aliyoitoa kuwa ni uwepo wa aliyekua Mgombea urais, Edward Lowassa
kuwa alihamia kwenye chama kwa kutofuata utaratibu.
Taarifa
kutoka ndani ya chama hicho zinasema kutokana na katiba ya chama,
Lipumba hatakiwi kurudi katika nafasi hiyo kwa kutengua kujiuzulu kwake
isipokuwa kama anahitaji nafasi hiyo achukue fomu upya kugombea nafasi
hiyo katika Mkutano Mkuu wa Taifa
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini