SAKATA la Kampuni ya Lugumi limesababisha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuagiza kupitiwa upya mikataba yote.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakuu
na waandamizi wa vyombo vya usalama vilivyopo chini ya wizara hiyo.
Kampuni
ya Lugumi iliyoingia mkataba wa Sh 37 bilioni na Jeshi la Polisi kwa
ajili ya kufunga mashine za kielektroniki za kuchukua alama za vidole
nchi nzima, haikutimiza matakwa ya mkataba wake baada ya kufunga mashine
14 tu kati ya 108 ilizotakiwa kufunga licha ya kulipwa asilimia 99 ya
fedha kwa mujibu wa mkataba.
Masauni
amesema, kutokana na kuwepo kwa utata wa mikataba, wizara imeagiza
mikataba yote kupitiwa upya na ile ambayo itabainika kuwa na kasoro,
itavunjwa.
“Mikataba yote ambayo majeshi haya yameingia ihakikiwe na ipitiwe upya ili iweze kurekebishwa na kazi hiyo iende haraka sana ili kuleta tija kwa wananchi wetu,” amesema Masauni.
Mbali
na hilo ameiagiza Idara ya Uhamiaji nchini kuhakikisha inawachukulia
hatua kali wale wote ambao wanaonekana kufanya kazi kinyume na misingi
ya jeshi hilo.
“Kuanzia
kesho naagiza kuhakikisha wanachukuliwa hatua wale wote ambao
hawaendani na kasi yetu ya utendaji wa kazi na kuwaleta vijana vijana
ambao wanaendana na kasi yetu ya hapa ni kazi tu.
“Kumekuwepo
na shida kubwa katika maofisa wetu wa Idara ya Uhamiaji wanaohusika na
mambo ya uchunguzi ambao wamekuwa wakienda katika baadhi ya makampuni
kufanya uchunguzi kama kuna watu ambao ni wahamiaji haramu lakini
hawafanyi kile ambacho wanatakiwa kukifanya.
“Changamoto
kubwa ipo katika Jiji la Dar es Salaam na kwa maana hiyo nimeagiza watu
hao waondolewe mara moja na hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe
haraka iwezekanavyo na (kesho) leo zoezi hilo liwe limekamilika” amesema Masauni.
Aidha
ameiagiza Idara ya Uhamihaji kuhakikisha inaimarisha ulinzi mipakani
ili kutibu tatizo la wahamihaji haramu wanaoingia kutoka nchi za jirani
na kukamatiwa katika maeneo ambayo siyo ya mipakani.
Masauni
amesema, licha ya kuwa kwa sasa nchi ipo shwari kalini jeshi la polisi
linakazi kubwa ya kuhakikisha linaimarisha ulinzi, na kufanya upelelezi
wa kina na kwa haraka pale yanapotokea mauaji au uharifu wa aina yoyote.
Kuhusu
masuala ya ajira ndani ya wizara hiyo ambazo serikali ilitangaza
kuzisitisha, Masauni amesema, kwa sasa baada ya wakuu wa idara zote
viongozi waandamizi kukaa, wamekubaliana kurejesha ajira hizo katika
Idara ya Uhamiaji na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
“Kwa
sasa idara ya uhamiaji ina nafasi za ajira 702 ambazo zinahitaji
kujazwa huku Jeshi la Zima moto na uhokoaji zinahitaji ajira 522.
“Kutokana
na hali hiyo na kwa kuzingatia kwamba idara hizo zilikuwa
hazijakamilisha ajira hizo wakati wa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16
zilikuwa hazijajazwa na hivyo kama ajira zingeendelea kusitishwa vijana
wengi wangekosa haki yao nab ado kuna upungufu.
“Vijana
wenye sifa sasa wanaweza kuanza kujiandaa kwa ajili ya kufanya maombi
pale ambapo nafasi hizo zitaanza kutangazwa katika vyombo vya habari” amesema Masauni.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini