Mchezaji mwingine wa kike wa Cameroon afariki. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Tuesday, May 10, 2016

Mchezaji mwingine wa kike wa Cameroon afariki.



Mlinda Mlango, Jeanine Christelle Djomnang
Jeanine Christelle Djomnang mwenye umri wa miaka 26, alianguka wakati wa mazoezi ya kupasha misuli kabla ya mechi ya Femina Stars Ebolowa Jumapili, ingawa sababu za kifo chake bado hazijajulikana na inasubiriwa taarifa ya kitabibu.
Kifo cha kipa huyo wa timu ya wanawake, kinafuatia kifo cha kiungo wa kimataifa wa Cameroon, Ekeng, aliyezimia wakati wa mechi ya Daraja la Kwanza Romania akiichezea timu yake, Dinamo Bucharest usiku wa Ijumaa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alianguka uwanjani bila ya kuguswa na mchezaji yeyote dakika ya 70 katika mchezo dhidi ya Viitorul, dakika saba tu tangu aingine akitokea benchi.
Ekeng alikimbizwa hospitali, lakini madaktari wakashindwa kuokoa maisha yake.
Vifo vya Djomnang na Ekeng vimewakumbusha miaka 13 iliyopita wapenzi wa soka wa Cameroon wakati kiungo wa zamani wa kimataifa wa timu hiyo, Marc-Vivien Foe alipofariki dunia akiwa ana umri wa miaka 28 baada ya kuanguka na kupoteza fahamu mwaka 2003 kwenye Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Mabara la FIFA mjini Lyon, Ufaransa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin