WAZIRI
Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa
amemtaka Mkuu wa Magereza mkoa wa Lindi, kuhakikisha hakuna mtuhumiwa wa
dawa za kulevya atakayetoweka katika gereza la mkoa huo.
Amesema
kuna watuhumiwa wa dawa za kulevya ambao wanahifadhiwa katika gereza la
mkoa wa Lindi hivyo ni vema akajiridhisha kama ulinzi na usalama wa
watuhumiwa hao umeimarishwa.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu, Majaliwa amemtaka mkuu wa gereza hilo kuwa makini
na baadhi ya zabuni wanazozitoa kutoka nje na kuhakikisha ulinzi
unaimarisha wakati wote gerezani hapo.
Waziri
Mkuu, Majaliwa aliyasema hayo jana (10 Aprili, 2016) wilayani Ruangwa
wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Lindi iliyowasilishwa
kwake na Mkuu wa mkoa huo, Godfrey Zambi.
“Mkuu
wa Magereza wa mkoa atembee gereza ambalo wanashikiliwa watuhumiwa wa
dawa za kulevya na aangalie mradi unaolenga kupeleka maji gerezani hapo
kama ni kweli au njia…,” alisema Waziri Mkuu, Majaliwa.
Aidha,
Waziri Mkuu, Majaliwa alimtaka mkuu huyo wa Magereza kujiridhisha kama
ulinzi na usalama wao umeimarishwa na kuhakikisha hakuna mtuhumiwa
anayetoweka.
Awali
akisoma taarifa kwa Waziri Mkuu, mkuu wa mkoa wa Lindi, Zambi alisema
matumizi ya dawa za kulevya hususan kwa vijana ni miongoni mwa
changamoto zinazoukabili mkoa huu ambapo wilaya ya Kilwa inaongoza kwa
kuwa na waathirika wengi.
Alisema
matumizi ya dawa hizo yanasababisha kupunguza kwa nguvu kazi kwani
watumiaji wengi ni vijana, hivyo alitoa wito kwa wananchi kushirikiana
na serikali katika kupiga vita matumizi ya dawa hizo kwa kuwafichua
wauzaji na watumiaji.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini