TANZANIA imetajwa kuwa inaongoza kwa kulima na kuzalisha ufuta Afrika huku ikishika nafasi ya tatu ya duniani.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa
Kilimo na Maendeleo, Naliendele, Dk Omary Mponda, alisema kuwa Tanzania
imefikia hapo baada ya jitihada kubwa zilizofanywa na serikali.
Jitihada
hizo zinafanyika kupitia watafiti wake wa masuala ya kilimo kwa
kutafiti na kugundua mbegu bora zinazostahimili ukame, magonjwa na
wadudu.
Mtaalamu
huyo ambaye pia ni mtafiti kiongozi na mratibu wa mbegu za mafuta,
alisema kwa sasa Tanzania inazalisha wastani wa tani 460,000 kutoka tani
38,000 zilizokuwa zikizalishwa mwanzoni mwa miaka ya 1980.
Alisema
kwa mujibu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO), Tanzania imepanda
kutoka nafasi ya saba kidunia mwaka 1998 hadi kufikia nafasi ya tatu
ikitanguliwa na India na Mayama.
“Hiki
kituo cha utafiti kilianza mwaka 1945 wakati huo kilikuwa
kinashughulikia korosho peke yake, lakini kufikia mwaka 1978 tulianza
kuingiza utafiti wa mbegu za karanga na ufuta ambapo mpaka sasa
tumeshagundua mbegu aina 12 ambazo wakulima wetu wanazitumia”, alisema.
Mtaalamu
huyo aliyebobea katika masuala ya utafiti wa mbegu za mafuta, alisema
kuwa zao hilo miaka ya nyuma lilikuwa linalimwa katika mikoa ya Kusini
ambayo ni Mtwara, Lindi na Ruvuma. Alisema kutokana na hamasa kubwa
inayofanywa na wataalamu wa kilimo, tayari mikoa kadhaa inalima zao
hilo.
“Huko
nyuma hata eneo lililokuwa likilimwa ufuta lilikuwa dogo sana, lakini
sasa ni zaidi ya hekta 650,000 zinalimwa ufuta nchi nzima…sasa haya ni
mafanikio makubwa na yanayopaswa kujivunia na hiyo inatokana na ugunduzi
huu wa mbegu bora”, alisema.
Ufuta
ni moja kati ya mazao yanayoongeza kipato kwa makusanyo ya ndani kwa
baadhi ya halmashauri za wilaya ikiwemo wilaya ya Liwale, Nachingwea na
Ruangwa mkoani Lindi ambapo kwa mujibu wa takwimu zilizopo Ruangwa,
msimu uliopita ilipata Sh milioni 400 kutokana na ushuru wa mauzo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini