Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua
Bw. Gelasius Gaspar Byakanwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoani
Kilimanjaro.
Taarifa
iliyotolewa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanzia tarehe 08 April,
2016. Bw. Byakanwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Antony Mtaka
aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Byakanwa alikuwa Katibu wa Rais Msaidizi Mwandamizi.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
08 Aprili, 2016
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini