Marais John Magufuli na Paul Kagame wakiwasha mwenye eneo la Gisozi
Rais wa Tanzania John Magufuli amesema mauaji ya kimbari sawa na yaliyotokea nchini Rwanda hayafai kuruhusiwa kutokea tena.
Akizungumza
mara baada ya kutembelea jumba la makumbusho mauaji ya Kimbari ya mwaka
1994, Rais Magufuli amesema amesikitishwa sana na mauaji hayo.
"Haitatokea
tena, hatuwezi kubadilisha yaliyopita lakini tunaweza kubadilisha mambo
ya sasa na yajayo, mauaji haya hayapaswi kutokea tena," amesema Dkt
Magufuli, kwa mujibuwa taarifa kutoka ikulu.
Rwanda
imekuwa ikiadhimisha kumbukumbu ya miaka 22 ya tangu kutokea kwa mauaji
ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu takribani 800,000.
Rais
Magufuli na mwenyeji wake Paul Kagame waliwasha mwenge utakaowaka kwa
kipindi cha siku 100 yaliyodumu mauaji ya kimbari ya Rwanda katika eneo
la makumbusho hayo Gisozi.
Mkuu wa
kitengo cha Rwanda cha kupambana na mauaji ya kimbari Dkt Jean Damascene
Bizimana, akihutubu wakati wa maadhimisho mafupi ya kukumbuka mauaji
hayo, amezihimiza nchi za Afrika Mashariki kubuni sheria za kufwatilia
na kuwadhibiti watu wanaoeneza itikadi za mauaji ya kimbari.
Tanzania na Rwanda zafungua ukurasa mpya
Amesema
nchi za Burundi na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo zilitoa hifadhi na
kushirikiana na wapiganaji wa kundi la FDLR wanaotuhumiwa kutekeleza
mauaji hayo.
Amesema
Rwanda imefurahishwa sana na taifa la Ujerumani kwa kuwakamata na
kuwahukumu vinara wa kundi hilo wanaoishi nchini Ujerumani kutokana na
mchango wao katika mauaji yanayotekelezwa na kundi hilo nchini Congo.
Viongozi hao wa FDLR ni Ignace Murwanashyaka aliyehukumiwa miaka 13 jela na Straton Musoni aliyehukumiwa miaka 8 jela.
Mwandishi
wa BBC aliyeko Rwanda Yves Bucyana anasema kutakuwa na wiki nzima ya
maombolezo kukumbuka waliouawa wakati wa mauaji hayo.
Shughuli za michezo na burudani zimepigwa marufuku huku bendera zikipepea nusu mlingoti.
Dkt
Magufuli amekuwa kwenye ziara rasmi ya siku mbili nchini Rwanda, ziara
yake ya kwanza nje ya nchi tangu kuingia madarakani Novemba mwaka jana.
Ameondoka Kigali na kurejea Dar es Salaam.BBC
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini