Kim Jong-un
Korea
Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kufanya majaribio ya mtambo wake
mpya, ambao unaweza kurusha makombora kutoka bara moja hadi jiingine,
katika juhudi za kuimarisha uwezo wake wa kufanya mashambulio dhidi ya
Marekani.
Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vinasema kuwa zoezi hilo liliongozwa na kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-un.
Jaribio
hilo ni katika harakati za hivi karibuni za utawala wa Pyongyang wa
kuunda zana za nuklia tangu ilipofanya jaribio lake la nne la makombora
ya nuklia January mwaka huu.
Hatua hiyo iliiushurutisha Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo vipya.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetoa wito kwa utawala wa Pyongyang kujiepusha na vitendo vyake vya uchochezi.BBC
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini