Obama
aliwaambia Wamarekani kwamba mageuzi anayoyatete ni kwa manufaa yao
wenyewe kwa kuwa yeye huu ni mwaka wake wa mwisho kukaa madarakani na
wala hana mpango wa kugombea.
Rais
Obama anataka watu wote wanaouza silaha washurutishwe kuwapekua na
kuchunguza historia ya watu wanaowauzia silaha.Kwa sasa, takwa hilo
hugusa tu wauzaji silaha waliosajiliwa.
Wauza
silaha ambao hawajasajiliwa, hutakiwa kuwauliza tu wateja wao iwapo
wamewahi kupatikana na makosa ya uhalifu au kama wana matatizo ya
kiakili.
Hatua hiyo ya Rais Obama imepingwa vikali na baadhi ya viongozi wakuu wa chama cha Republican wanaosema inaingilia uhuru wa kikatiba wa Wamarekani.
Rais Barack Obama alitokwa na machozi jana alipokuwa akitetea kufanyiwa mabadiliko kwa sheria za udhibiti wa silaha nchini Marekani ili kupunguza idadi ya watu wanaoshambuliwa na kuuawa kwa Risasi nchini humo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini