
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Peter Kakamba amesema watu hao
raia wa Ethiopia wamekamatwa katika kituo cha ukaguzi wa magari Igumbilo
manispaa ya Iringa wakati jeshi la polisi mkoani hapa likiwa kwenye
operesheni ya kawaida limewakamata raia hao pamoja na mtu mwingine mmoja
anayedaiwa kuwa msindikizaji lakini haikufahamika kama alikuwa
akisindikiza magazeti ama alikuwa anasindikiza raia hao wa Ethiopia.
Katika tukio lingine kamanda Kakamba amesema mnamo siku ya tarehe
25 gari lenye namba za usajiri T.275 BMW lilikuwa likiendeshwa na Manase
Alen mwenye umri wa miaka 29 liligongana na pikipiki iliyokuwa imepakia
abiria wawili maarufu mishkaki ambayo haikuweza kufahamika namba zake
kutokana na kuharibika vibaya iliyokuwa ikiendeshwa na Filbert Mmale na
kuwaua papo hapo dereva huyo wa pikipiki na abiria wawili Emmanuel
Kitosi miaka 30 na Hamisi Sigara wote wakazi wa Mseke mkoani Iringa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini