Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
11 Januari, 2016 amemtembelea na kumpa pole Waziri Mkuu Mstaafu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Frederick Sumaye ambaye
amelazwa katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa
Frederick Sumaye alilazwa katika Taasisi hiyo siku nne zilizopita kwa
matibabu ya moyo na madaktari wanaomtibu wamemhakikishia Rais Magufuli
kuwa anaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati alipofikishwa katika
Taasisi hiyo.
Pamoja na kumpa pole, Rais Magufuli pia amemuombea apone haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
Akizungumza mara baada ya kuonana na Rais, Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye amemshukuru Rais Magufuli kwa kwenda kumuona na kueleza kuwa kitendo hicho kimeonesha jinsi alivyo na upendo wa dhati na anavyowajali watu wake.
Kuhusu hali yake, Mheshimiwa Sumaye amesema anaendelea vizuri, anapata matibabu mazuri na kwamba kwa kuwa hali yake ni nzuri anatarajia kuruhusiwa kuondoka hospitali hapo baada ya muda mfupi.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
11 Januari, 2016

Dkt
John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu Mhe
Freredick Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
salaam Januari 11, 2016
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe
Freredick Sumaye na Mama Esther Sumaye alipokwenda kumjulia hali Waziri
Mkuu Mstaafu huyo Mhe Freredick Sumaye katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam
Januari 11, 2016
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini