Mstakabali wa Van Gaal Old Trafford umekuwa ukichunguzwa katika wiki za karibuni na Mholanzi huyo atakuwa kwenye wakati mgumu endapo United itatolewa kwenye Komba la FA na Derby County siku ya Ijumaa usiku.
Lakini mbishi Van Gaal amedai kwamba daima anapenda kumaliza mkataba wake, ambao utamalizikia majira ya joto 2017, na hivyo anapambana kwa ajili ya kibarua chake.
“Kila mtu anajua nimesaini mkataba wa miaka mitatu,” alisema Van Gaal. Ni mchakato, sio mchezo mmoja, na nataka kuendelea hadi mwisho. Kama nisingekuwa tayari kufanya hivyo, sidhani kama ningeanzia hapa. Ninapambana daima.”
Kocha wa Old Trafford alikaribisha kuungwa mkono na mkuu wa United Ed Woodward na familia ya Glazers lakini, kiudadisi, alisema msaada wao umempa shinikizo la kupambana zaidi.
“Bila shaka nina furaha na ushirikiano wa Ed Woodward na Glazers,” alisema. Lakini wakati bodi ikiwa na imani na wewe, shinikizo linakuwa kubwa zaidi kuliko wakisema hii ndio mechi yako ya mwisho. Hivyo imani yako inashuka na unaweza kupambana nayo. Na unapopambana unakuwa na lengo kubwa ikiwa bado wanakuunga mkono.”
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini