Jaji wa mahakama kuu ya Tanzania kitengo cha ardhi Panterine Kente
ambaye anasikiliza kesi hiyo ametaja tarehe hiyo ambapo kesi ya msingi
itaanza kusikilizwa baada ya mabishano ya kisheria ya pande zote mbili
serikali na mawakili wa watuma maombi kutolewa uamuzi na jaji huyo.
Kesi hiyo ilifunguliwa na mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh Abdalah
Mtulia ambayo inawakilisha wananchi zaidi ya mia sita ambao nyumba zao
zinatakiwa kubomolewa kutokana na kujengwa mabondeni na nyingine maeneo
yasiyoruhusiwa.
Hata hivyo mapema wiki iliyopita jaji Kente alitolea maamuzi kesi
hiyo kwa kuweka zuio la kutobomoa nyumba ambazo wamiliki wake wamepeleka
maombi mahakamani ambapo alisema mahakama imezingatia maelezo toka
pande zote mbili kwa kuangalia madhara watakayopata wananchi kwa
kutekelezwa kwa zoezi hilo.
Aidha katika maelezo yake wakati wa kusoma huku hiyo jaji Kente
alisema zuio hilo linawahusu watuma maombi tu hivyo serikali itaendelea
na uwekaji wa alama za X na ubomoaji wa nyumba zilizopo sehemu hatarishi
na sehemu zisizoruhusiwa.
Wakati huohuo kesi ya nyumba ya mchungaji wa kanisa la Assemblies
of God Mikocheni, Dk. Getrude Lwakatare ambayo ilikuwa ibomolewe na
kuwekewe zuio na mahakama hiyo nayo itaanza kusikilizwa Januari 21 mwaka
huu.
Kesi hiyo ambayo iko kwa jaji John Mgeta maombi yake yaliwasilishwa
na wakili wa mama Lwakatare ambapo inadaiwa mwaka 2011 NEMC ilitoa
notisi ya kuvunja nyumba hiyo kwa madai kuwa ujenzi wake unaziba mto
Ndumbwi na uko jirani na mikoko.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini