Askofu Pengo: "Muhimbili Panatosha na Nimeridhika Na Huduma Za Hapa Sihitaji Nje Ya Nchi. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Thursday, January 7, 2016

Askofu Pengo: "Muhimbili Panatosha na Nimeridhika Na Huduma Za Hapa Sihitaji Nje Ya Nchi.


Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki  la Dar es salaam,Muadhama, Kardinali  Pengo amesema kwamba ameridhishwa na huduma za afya zinazotolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), hivyo itakuwa ni vigumu kwa Serikali kumshawishi kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana  na Askofu Pengo ambaye amelezwa katika  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya  MNH  jijini Dar es Salaam kuanzia  Januari Mosi, mwaka  2016 hadi sasa mara baada ya kuzungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  ambaye alimtembelea  jana  mchana  ili kuweza kufahamu maendeleo ya afya yake.

“Ninapenda kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania  na kuwaondoa hofu kuwa hali ya Baba Askofu Pengo imeimarika na  anaendelea vizuri, hajawekewa oxygen wala hajalazwa katika wodi ya uangalizi maalum(ICU) na ameridhika na huduma zinazotolewa,.

“Ameridhika  na  huduma zinazotolewa za moyo, itakuwa ni vigumu sisi kama Serikali kumshawishi kwenda kutibiwa nje ya nchi, ” alisema  Waziri huyo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin