SERIKALI
imepanga kupeleka Sh. 18.77 bilioni kila mwezi katika shule za
sekondari na msingi kwa ajili ya kugharamia elimu ili kutekeleza dhana
ya elimu bure kuanzia Januari, 2016.
Taarifa
hiyo ilitolewa Mjini Dodoma jana na Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa elimu bure.
Alianisha
fedha zitakazotolewa na Serikali kwa ajili ya kugharamia elimu ni
pamoja na gharama za mitihani ya kidato cha nne ambazo zitatolewa moja
kwa moja na Serikali katika Baraza la Mitihani (Necta).
“Serikali
itatoa pia ruzuku ya uendeshaji wa shule Sh. 10,000 kwa shule za msingi
na Sh. 25,000 kwa shule za sekondari kwa kila mwanafunzi kwa mwaka.
“Vilevile
itatoa Sh. 1,500 kwa siku kwa mwanafunzi kwa shule za msingi na
sekondari kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi wanaokaa bweni,” amesema.
Simbachawene
amesema pia Serikali itatoa fedha kwa ajili ya fidia ya ada Sh. 20,000
kwa kila mwanafunzi wa shule ya kutwa na Sh. 70,000 kwa mwanafunzi wa
sekondari kwa mwaka.
Amesema
fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule zitasaidia pia uendeshaji wa
shule za hosteli ikiwemo gharama za chakula, mlinzi, mpishi, umeme na
maji.
Aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri husika kuhakikisha fedha hizo zinafika kwa wakati na zinatumika kwa kazi iliyokusudiwa.
Simbachawene
amesema majukumu ya wazazi pamoja na mambo mengine yatakuwa ni kununua
sare za shule, vifaa vya kujifunzia, gharama za matibabu, nauli, gharama
za chakula kwa wanafunzi wa shule za kutwa na kununua magodoro, shuka,
vifaa vya usafi binafsi kwa wanafunzi wa bweni.
“Natoa
wito kwa viongozi wote wakiwemo wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na
wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa kusimamia utekelezaji wa
elimu bila malipo,” amesema.
Aidha,
Simbachawene aliziagiza halmashauri na mikoa ambayo haikufanya vizuri
katika mitihani ya darasa la saba kujieleza sababu za kutofanya vizuri.
“Iwapo itathibitika kwamba kuna wahusika walizembea kutimiza majukumu yao wachukuliwe hatua zinazostahili.
“Nawaagiza
pia wakurugezi mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma kwamba ifikapo Februari
15 mwakani wawe wamekamilisha miundombinu ya shule ili wawewezeshe
wanafunzi 12,647 waliosalia kujiunga na elimu ya sekondari wanaenda
shule,” amesema.
Simbachawene
pia alizitaka kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya
kuwachukulia hatua za kisheria watu watakaosababisha wanafunzi kukatisha
masomo kwa utoro na mimba pamoja na wale waliooa watoto wa kike.
‘’Tusifanye
kazi kwa mazoea, tunatakiwa tuendane na kasi ya Rais John Magufuli ya
kufanya kazi kuwasaidia wananchi hasa katika sekta ya elimu,’’ amesema.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini