Na: Frank Shija, MAELEZO
Ukubwa
wa deni la taifa siyo jambo linaloweza kusababisha kuyumba kwa uchumi
wa nchi, kinachooneka ni kuendela kuaminiwa kwa Tanzania ndani na nje ya
nchi jambo linalopelekea tuna pata fursa ya kukopesheka kwa ajili ya
miradi ya maendeleo.
Hayo
yamebainishwa na Mchambuzi wa masuala ya kiuchumi, Profesa Haji Semboja
alipofanya mahojiano maalum na mwandishi kutoka Idara ya Habari,
MAELEZO kuhusu hali ya uchumi ilivyo kutokana na ongezeko la deni la
Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
“Ukubwa wa deni la taifa siyo mzigo mbaya, ni mzigo wa kimaendeleo. Unnecessary devil” Alisema Profesa Semboja.
Aliongeza
kuwa kutokana kwa imani waliyo nayo wahisani ndani na nje ya nchi ndiyo
maana washirika wetu wanatukopesha fedha kwa ajili ya miradi ya
maendeleo kama ambavyo tumeshuhudia ujenzi wa Daraja la Kigamboni, hivi
karibuni tutanufaika na usafiri wa ndege”. Alisema Profesa Semboja.
Aidha
amempongeza Rais wa Awamu ya Tano Mhe. Dkt. Jonh Pombe Joseph Magufuli
kwa hatua alizochukua za kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma kwa
kuondoa safari za nje zisizo za rasmi pamoja na kupiga vita vitendo vya
rushwa.
Semboja
aliendelea kusema kuwa kinachofanyika hivi sasa ni Serikali ya awamu ya
Tano kulipa madeni ya watangulizi wake huku ikitekeleza miradi ya
maendeleo jambo linaloongeza imani miongoni mwa wahisani.
Hata
hivyo alionya juu ya matumizi mabaya ya rasilimali fedha kuwa
zinasababisha kushindwa kutekeleza wajibu wa kulipa deni kwa wakati na
kupelekea kulimbikiza madeni jambo ambalo si sahihi.
Alitajaa
baadhi ya matumizi mabaya ya fedha kuwa ni pamoja na safari za nje na
ndani ya nchi zisizokuwa na tija, ulevi, kupelekea fedha katika miradi
isiyopangwa na mengine.
Wananchi
wametakiwa kutoyumbishwa na waelewi kuwa kupitia fedha zinazokopwa
wanufaika wakuu ni wananchi wenyewe, mfano fedha zitakazo tumika kujenga
Nyumba za Magomeni ambazo Mhe. Rais amehaidi waliokuwa wakazi wake
kuishi bila kulipia kwa kipindi cha miaka mitano zikitokana na mikopo
hiyo wananufaika.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini