Serikali
ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inaendelea kukutana na wadau tofauti
wanaohusika na masuala ya uchumi katika kuhakikisha uchumi wa nchi
unaendelea kukua.
Hayo
yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la
Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe mijini Dodoma aliyetaka kujua hali ya
uchumi ilivyo kwa sasa hapa nchini.
Waziri
Mkuu amesema kuwa lengo kuu la Serikali ya awamu ya tano ni
kuhakikisha uchumi wa nchi unaongezeka kupitia nyanja tofauti kwa
kushirikiana na taasisi za fedha zilizopo ili kufikia uchumi wa kati
kama ilivyoanishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza
kuhusu suala la midororo wa upokeaji wa mizigo katika bandari nchini,
Waziri Mkuu amesema kuwa mdororo huo umetokana na kupungua kwa kiasi cha
mizigo na kushuka kwa uchumi duniani.
Katika
suala ya mauaji yaliyotokea Tanga, Mwanza na Vikindu, Waziri Mkuu
amesema kuwa usalama wa wananchi utaendelea kuimarishwa huku serikali
ikiahidi kupambana vitendo vya mauaji kwa raia na askari katika maeneo
mbali mbali nchini.
“Serikali
imesikitika sana na jambo hili la mauaji hivyo itahakikisha wauaji hao
wanawekwa katika mikono ya Sheria na kuongeza ulinzi kwa maeneo yote
nchini kwa kuanzia ngazi ya vitongoji” alifafanua Waziri Mkuu.
Mbali na hayo Waziri Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika kuthibiti matukio hayo.
Kuhusu
suala la uwepo wa tozo katika zao la korosho swali limeibuliwa na
Mbunge wa viti maalumu Mhe.Riziki Lulida (CUF), Waziri Mkuu Majaliwa
amesema kuwa Serikali imeshatoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya
kusimamia uondoaji wa Tozo zisizo na maana katika zao la korosho.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini