Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Lameck Nchemba amesema hakuna shamba
lenye thamani ya maisha ya binadamu na kuwataka wakulima na wafugaji
kutatua migogoro yao kwa kufuata sheria na kuacha kujichukulia sheria
mkononi.
Mwigulu
ameyasema hayo Bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza kutoka kwa
Mbunge wa Mikumi kupitia (CHADEMA) Joseph Haule aliyetaka kujua hatua
za serikali katika kudhibiti mauaji ya wakulima na wafugaji yanayotokea
mara kwa mara katika jimbo lake na maeneo mengine nchini.
Katika
swali lake Mbunge Haule ametaja baadhi ya mifano ya mauaji katika jimbo
lake hususani eneo la Tindiga ambapo mauaji yamekuwa yakifanyika mara
kwa mara huku serikali ikitoa matamko ambayo hayajazaa matunda.
Waziri
Mwigulu Nchemba amesema katika kijiji ambacho mauaji yatafanyika jeshi
la polisi litakamata vijana wote wenye nguvu na kuwafikisha kwenye
vyombo vya sheria ili wahusika waweze kubainika.
“Naliagiza
Jeshi la Polisi kuwakamata vijana wote wenye nguvu katika kijiji
ambacho mauaji yatafanyika ili wahusika wapatikane na kama magereza
zikijaa vibaka walioiba vitu vidogovidogo waachiwe ili hao ambao
wamesababisha mauaji wawekwe humo hatuwezi kufananisha maisha ya
binadamu na mifugo au shamba” Alisema Waziri Mwingulu.
Awali
katika swali hilo Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. William
Ole Nasha aliwataka wafugaji na wakulima kuepuka kutumia hasira ambazo
zinapelekea kugharimu maisha ya watu kwani serikali haitasita
kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini