KWA NINI NILIAMUA KUWA MJASIRIAMALI?SOMA HAPA UPATE MAJIBU. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Saturday, August 13, 2016

KWA NINI NILIAMUA KUWA MJASIRIAMALI?SOMA HAPA UPATE MAJIBU.


                                    Habari msomaji wangu karibu tena kwenye muendelezo wa makala zangu za ujasiriamali ili tupeane ufahamu juu ya kujitoa ktk sehem moja kwenda ktk sehe nyingine bora kimaisha.Leo ngoja nianze ivi MJASIRIAMALI WA LEO NI TAJIRI WA KESHO kuna tofauti kubwa sana kati ya mjasiriamali na mfanyabiashara
japo wapo watu wengi ambao wanafanyabiashara halafu sio wajasiriamali,mjasiriamali ni mtu ambaye hutumia rasilimali zinazomzunguka ili kujiingizia kipato na ni mtu ambae anachuua hatari (risk) anafanyabiashara zaidi ya moja, sasa wewe unakibiashara kimoja tu sijui kikifirisika unafanyaje?,na duniani tuna rasilimali kama nyingi   WATU,MAJI.ARDHI,MISITU,  GESI,MADINI       hizi ndizo rasilimali ambazo zilizotuzunguka ambazo kila mtu anatakiwa kuzitumia na sio kufungua tu duka ukae useme we mjasiriamali lazima ujiulize je usipofungua duka unawezakupata pesa kama hata usipofungua unaweza basi we ni mjasiriamali maana kipo kikundi cha watu wanafanya kazi kwaajili yako.lakini pia watu wengi hupenda kuniuliza umewezaje kuwa mfanyakazi na pia mjasiriamali ikiwa wengine wanashindwa? unajua wafanyakazi wengi niwavivu wa kufikiria akili zao zooote zinawatuma wapate pesa wakafungue maduka ndio wafanye biashara  mishahara yenyewe midogo matumizi kibao,kumbe wamesahau wanaweza anzia kwenye mazingira yale yale ya kazi kuwa wajasiriamali na baadae , kuwa wafanyabiashara wakubwa acha mawazo mgando rafiki unaweza anzia ofisini kwako hapo hapo na kuna kina mama nyumbani wanafikiri kuwa mjasiriamali hadi upate mtaji na kuendelea kukaa majumbani bila sababu usijali kama kweli unandoto kubwa za kubadilisha maisha yako nitafute nikuelekeze biashara ambayo waweza anza kufanya taratiibu ukaingia moja kwa moja kuwamjasiriamali mkubwa.
Niliamua kuwa mjasiriamali kwa sababu zifuatazo zisome kwa umakini ukiona zinakufaa basi waweza nitafuta nikakuonyesha wapi uanzie na wewe uwe mtu tofauti.

  1. UHURU WA MUDA                                                                                                                          Kiukweli huwa nachukizwa saana na swala la kuamka asubuhi saana kwenda kazini halafu mbaya zaidi ukifika kazini unawaza muda wa kusaini kwa hiyo hata kama iwe umekutana na foleni sehemu halafu ukachelewa kazini boss hakuelewi yeye anataka uwahi lkn pia natumia muda mwiingi saana kufanya kazi lkn ukiangalia mshahara na jinsi unavyofanya kazi haviendani,nikakaa nikafikiri hivi nifanye nini ili siku moja nisiwe na hizi adha za kuamka asubuhi ili na mimi nimiliki biashara yangu.hapo ndipo nilipopata wazo la kuwa mjasiriamali najua haikuwa kazi rahisi kuamua maana wafanyakazi ulishazoea ukitoka kazini unaenda nyumbani kupumzika kuangalia TV lkn ilibidi ule muda wangu wa ziada nianze kuutumia kujifunza ujasiriamali ili nimiliki biashara yangu mwenyewe.
  2. UHURU WA KIFEDHA                                                                                                                    Hakuna kitu ambacho kinaniudhi mimi kama inapotokea shida halafu huwezi ihimili hadi mshahara utoke,kiukweli mishahara ya kitanzania ni kama period inakuja mara moja kwa mwezi na haikai siku tano ukiangalia hata wewe ambae unafanya kazi leo ikifika tarehe 15 tayali huna hela yaani hata mtu aje aseme kunatatizo la kutoa elfu hamsini lazima upate kizunguzungu kwanza,nikasema hapana huu ni ujinga hivi kwanini nisitumie muda wangu wa ziada kuwa mjasiriamali ili nimiliki biashara zangu mwenyewe nikaanza kujitesa kwa kutumia muda wangu wa ziada kujifunza biashara hadi nikaweza.kwasababu nilikuwa nataka uhuru wa kifedha yani kwenye shida saa yoyote niwe tayali kukidhi rafiki acha kuzubaa hata wewe unaweza hebu fikiria muda wako wa ziada unautumiaje mbona unajifanya kuwa masikini amka wewe maisha yamebadilika rafiki,njoo tuyakomboe maisha yetu.
  3.       NIWASAIDIE WATU  WENGINE                                                                                       Hautaweza kufanikiwa katika maisha yako mpaka uwasaidie watu wengine (IF YU WANT TO GET WHAT YOU WANT YOU HAVE TO HELP OTHER PEOPLE TO GET WHAT THEY WANT)    Hapa ndipo watu weengi hufa wakiwa masikini bila wao kujua ndugu yangu kama hauko tayali kuwasaidia wengine usifikirie kabisa kufanikiwa,hakuna kitu ambacho ambacho kilikuwa kinaniumiza kichwa kama hicho yani nilikuwa sipati usingizi nikifikiria hivi nifanye nini ambacho tawasaidia watu wengine ukiangalia kazi yangu siwezi kuwasaidia watu wengine nao maisha yao yawe bora lkn lengo langu kuwasaidia watu wengine weengi nikaja kugundua ili niwasaidie watu wengine lazima niwe mjaisiriamali ndio taweza kuwasaidia watu wengine nashukuru Mungu sasa nawasaidia watu wengine maisha yao yanabadilika kifikra na kipesa na sitachoka.Hebu jiulize msomaji wangu siku ukiondoka hapa duniani watu watasema nn kuhusu wewe? upo tayali ufe kama ulikuwa haupo yani familia yako tu ndo ijue mama leo kafa au baba leo kafa,Hutaki kufa ukiwa mtu maarufu.hebu ibadilishe prfile yako leo na kama hujui jinsi ya kuibadilisha njoo takuonyesha.SIMAMA LEO UFANYE JAMBO INAWEZEKANA.(WAKATI NI UKUTA )Wasaidie watu wengi nawe utajisaidia ili kuyafanya hayo kuwa mjasiriamali,
  4. UHURU WA KIHISIA                                                                                                                      Hapa ndipo wengi huteseka hebu jiulize mara ngapi umeenda kazini ukiwa hutaki kwenda kazini yaani unaamka mwili umechoka huenda hata unaumwa lkn kwa kuwa kazi umeajiriwa lazima uende tu kazini,au jiulize wangapi leo wameshazeeka na hawapendi kuwa wafanyakazi lkn inabidi wawe wafanyakazi kwa kuwa hawana cha kufanya? ni wengi niliamua kuwa mjasiriamali ili niwe na uhuru wa kihisia ili siku nikiwa sijisikii nalala tu nyumbani na hakuna wa kuniuliza.Hujachelewa rafiki hata wewe unaweza kuyafanya hayo.                                                                                                                   Kama nawewe fikra zako ni kama hizo au unamawazo kama hayo basi usijali nitafute kwa namba zangu hapo juu nikuonyeshe cha kufanya au ni mjasiriamali lkn ungependa tubadilishane mawazo karibu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin