Watu
watano wamenusurika kufa wilayani Songea mkoani Ruvuma baada ya roli
lililoegeshwa kuporomoka bila dereva na kugonga maduka na nguzo za umeme
na kusababisha taharuki kubwa na kujeruhi watu wawili waliolazwa katika
hospitali ya mkoa wa Ruvuma huku shughuli zikisimama na barabara ya
Songea-Mbinga kulikotokea ajali ikifungwa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wanaelezea jinsi tukio
lilivyotokea na namna roli hilo lililoporomka bila dereva na kuparamia
maduka na kugonga nguzo za umeme mjini Songea na kujeruhi watu wawili na
kugonga kwenye duka la vifaa vya umeme la Bw. Henry Tweve aliyekuwemo
ndani ya duka hilo na watu wengine wawili ambapo pia limejeruhi watu
wengine wawili kabla ya kugonga duka hilo.
Baadhi ya wananchi wamelaani kitendo cha kuegesha maroli mjini
wakatiu serikali ilipiga marufuku maroli kuegeshwa mjini na kuitaka
serikali kusimamia sheria zake ilizojiwekea za kuhakikisha maroli
hayaegeshwi mjini ili kuepesha ajali kama hizo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Bw. Zuberi Mwombeji alipopigiwa
simu yake ya mkononi ilipokelewa na mlinzi wake aliyesema yuko msibani
huku waathirika wa ajali hiyo wakieleza hasara walizozipata.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini