Wananchi wa Kagera waipongeza serikali ya awamu ya 5 kwa kuonyesha adhima ya kununua meli mpya. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Saturday, June 11, 2016

Wananchi wa Kagera waipongeza serikali ya awamu ya 5 kwa kuonyesha adhima ya kununua meli mpya.



Baadhi ya wananchi katika mkoa wa Kagera wamepongeza serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutenga kiasi cha fedha kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya ununuzi wa meli mpya mbili zitakazotoa huduma ya usafiri ndani ya ziwa Victoria na kuzifanyia matengenezo makubwa meli zilizosimamisha huduma kutokana na ubovu za MV.Serengeti na MV. Victoria.
Wananchi hao wakizungumza na ITV kwa nyakati tofauti wakati wakitoa pongezi kwa rais huyo wamesema uamzi wa serikali ya awamu ya tano wa kutenga bajeti ya kununua meli mpya na kukarabati meli mbovu unamdhihirisha wazi rais wa awamu hiyo alivyo na mapenzi ya dhati kwa wananchi waliomchagua kwa kuwa baadhi ya marais wa serikali za awamu zilizopita walitoa ahadi za ununuzi wa meli bila kuzitimiza.
Kwa upande wake Abdul Ziadi, mwenyekiti wa watoa huduma katika bandari ya Bukoba amesema kusimamishwa kwa meli za MV. Serengeti na MV. Victoria kuwa kumewaathiri sana wananchi wengi waliokuwa wakitegemea safari za meli hizo katiika kujipatia kipato na katika kusafirisha bidhaa zao hivyo akaeleza kuwa dhamira ya Dkt. Magufuli ya kununua meli mpya na kutengeneza zile za zamani kuwa inapaswa kupongezwa na kila mtu.
 
Mv. Serengeti ndio ilikuwa meli pekee iliyokuwa ikitoa huduma za usafiri ndani ya ziwa kati ya bandari ya Bukoba na Mwanza ilisimamisha Machi 21, mwaka huu kutokana na ubovu, usafiri wa meli hiyo kila wiki ulikuwa ikiingia kampuni ya taifa ya huduma za meli zaidi ya shilingi milioni 36.
 
 
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin