TAKURURU Waendelea Kuchunguza Waliopokea Pesa za ESCROW..Mkurugenzi Asema Wasizani Wapo Salama. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Tuesday, June 28, 2016

TAKURURU Waendelea Kuchunguza Waliopokea Pesa za ESCROW..Mkurugenzi Asema Wasizani Wapo Salama.



Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola amesema watu waliopokea mgawo wa fedha zilizotoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, hawako salama kwani anaendelea kuchunguza nyaraka.

Amesema uchunguzi wa sakata hilo la uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni kutoka kwenye akaunti hiyo unahitaji umakini mkubwa, ukikamilika wote watakaobainika watachukuliwa hatua.

 Mawaziri wawili (Profesa Sospeter Muhongo na Profesa Anna Tibaijuka), waliwajibika kutokana na sakata hilo, viongozi wa kamati za Bunge (Andrew Chenge, William Ngeleja na Victor Mwambalaswa) kuvuliwa madaraka, wanasiasa kufikishwa mbele ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi na watumishi wengine kufikishwa mahakamani.

Chenge na Profesa Tibaijuka waliwajibishwa kutokana na kuonekana wameingiziwa Sh1.6 bilioni kila mmoja kwenye akaunti zao, Ngeleja (Sh40.4 milioni), wakati Mwambalaswa aliwajibika kutokana na mgongano wa kimaslahi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin