Simu za bandia zazagaa mkoani Mtwara. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Thursday, June 16, 2016

Simu za bandia zazagaa mkoani Mtwara.



Licha ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutoa tangazo la kuzima simu bandia nchini, wafanya biashara wa bidhaa za simu za kiganjani mkoani Mtwara bado wanazo simu nyingi bandia katika maduka yao.
Wakizungumza na East Africa Radio mkoani humo, wafanya biashara hao ambao baadhi yao wamepatiwa semina ya kutoa elimu kwa umma juu ya ufahamu wa rajisi ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani, iliyoendeshwa na TCRA, wamesema hawajui kwa kuzipeleka simu hizo ambazo zitawasabashia hasara kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake, Mhandisi wa Mfumo rajisi wa namba za utambulisho wa simu kutoka TCRA, Imelda Salum, amesema simu hizo hazitokuwa na faida tena licha kuendelea kuwapo madukani.
Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, amevitaka vyombo vya usalama mkoani humo kutosita kuwachukulia hatua watu watakaobainika kufanya uvunjifu wa sheria za matumizi ya mitandao ya mawasiliano, huku kamanda wa polisi mkoani humo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Henry Mwaibambe akiwataka TCRA kuboresha mfumo wa huduma za usajili wa namba za simu.
Zoezi la kuzima simu bandia nchini linatarajiwa kutekelezwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA leo June 16 ifikapo saa 6 usiku.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin