Nyumba
moja iliyopo mtaa wa Kiseke Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza imeteketea
kwa moto leo asubuhi na kuunguza vitu vingi huku wakazi wa nyumba hiyo
wakinusurika.
Taarifa zinaarifu kuwa, nyumba hiyo imewaka moto baada ya mmoja wa
watoto wa familia hiyo kuamka asubuhi na kumwaga mafuta ya taa katika
moja ya chumba cha nyumba hiyo na kisha kuwasha moto
Imeelezwa
kuwa, kijana huyo ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya akili amekuwa
akiwatishia kwa muda mrefu kuwachoma moto lakini wamekuwa wakimpuuza
kutokana na matatizo yake ya akili
Baada
ya kumwaga mafuta na kuwasha moto, kijana huyo alitoweka na
kuwafungia ndugu wengine ndani ambapo majirani walifanikiwa kuwahi
kuwaokoa
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini