Kamati
ya bunge ya bajeti imeishutumu serikali kuwa imekuwa haiiamini na
kwa kiasi kikubwa katika bajeti ya mwaka huu ushauri ambao imekuwa
ikitoa umekuwa ukipuuuzwa hatua ambayo imesema ni ishara ya
kutaka kulirudisha bunge kuwa muhuri katika kuidhinisha bajeti ya
mwaka huu.
Akisoma hotuba ya kamati hiyo bungeni mwenyekiti wake mh hawa
ghasia amesema serikali imekuwa haipokei ushauri wa vyanzo vipya vya
mapato ambavyo wamekuwa wakishauri.
Kwa upande wake naibu waziri kivuli na msemaji mkuu wa kambi ya
upinzani bungeni katika wizara ya fedha na mipango mh.david silinde
amesema hawana tatizo na mpango wa serikali wa kutaka kukata kodi
asilimia tano kwenye kiinua mgongo cha wabunge ambapo kambi hiyo
ya uapinzani baada ya kuwasiliasha hotuba yao pia walifanya mkutano na
waandishi habari na kufafanua kuhusu bajeti hiyo , mh james mbatia
anasema.
Baadhi ya wabunge wakichangia bajeti hiyo wamesema bajeti
iliyowasilishwa imegusa sehemu nyingi na itaweza kuwafikisha
wananchi jambo la muhimu ni kila mtu kuhakisha anajitahidi kulipa
kodi ili bajeti iweze kutekelezeka.
Katika hatua nyingine naibu spika dk tulia ackson ameielekeza
kamati ya haki maadili na madaraka ya bunge kinga na maadili ya
bunge kuchunguza na kutolea uamuzi kitendo kinachodaiwa kufanywa na
mh joseph mbilinyi mbunge wa mbeya mjini cha kuonyesha kidole la kati
hatua ambayo imetafisiriwa kama ni kulidhihaki bunge.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini