Jukwaa
la katiba Tanzania limemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt John Magufuli kutaja tarehe rasmi ya kuanza mchakato wa upatikanaji
wa katiba mpya katika serikali ya awamu ya tano ili kuanza mapema katika
mwaka wa fedha unaoanza julai mosi mwaka huu.
Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa bodi ya jukwaa la
katiba Bw.Deusi Kibamba amepongeza jitihada za Rais Magufuli za kubana
matumizi serikalini hivyo basi ametumia fursa hiyo kuomba mchakato wa
upatikanaji wa katiba mpya kuanza kutokana na kugharimu fedha kiasi cha
zaidi ya bilioni 100 bila kufikia malengo.
Katika hatua nyingine Ebron Mwakagenda amesema wananchi wako na
uhitaji wa katiba mpya iliyoainisha mambo muhimu yanayowagusa na kutatua
changamoto walizo nazo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini