MBUNGE
wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT-Wazalendo) na wenzake wawili, jana
wamehojiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na
Madaraka ya Bunge, George Mkuchika kwa kufanya fujo bungeni kuhusu suala
la Bunge kutorushwa ‘live’.
Mbali
na Zitto, wengine waliohojiwa ni pamoja na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee
(Chadema) na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema). Wabunge
hao walihojiwa kwa tuhuma za kufanya fujo bungeni wakati ilipotolewa
hoja ya Bunge kutorushwa moja kwa moja ‘live’, akiwa pamoja na wabunge
wawili; Mdee na Heche.
Chanzo
cha uhakika kutoka ndani ya kamati hiyo, kimesema Zitto alihojiwa na
kamati hiyo kwa muda wa zaidi ya saa moja kwa makosa mbalimbali, ikiwamo
kufanya fujo bungeni Januari 27, mwaka huu.
Taarifa
hizo zilieleza kuwa Zitto alifanya fujo hizo baada ya Mwenyekiti wa
Bunge, Andrew Chenge, kuahirisha kujadili hoja ya serikali
iliyowasilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye, kuhusu Bunge kutorushwa ‘live’.
Hatua
hiyo inatokana na hoja iliyowasilishwa na Zitto aliyetaka kuahirishwa
kujadili hotuba ya Rais kutokana na kauli ya Waziri Nape ya kutorushwa
matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.
Zitto,
alihojiwa na kamati hiyo ya Mkuchika kwa kilichoelezwa alisimama na
kuomba mwongozo kuhusu jambo ambalo limekwishatolewa uamuzi kinyume na
Kanuni ya 72 (1) na 68 (10 ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari
2016.
Mbali
na hilo pia anadaiwa kusimama na kuzungumza bila utaratibu kinyume na
Kanuni ya 60 (2) na 12 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, jambo ambalo
lilileta fujo na kuvunja shughuli za Bunge.
Katika
barua za mwito zilizosainiwa na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah,
Mei 12, mwaka huu, inaelezwa kwamba pamoja na mambo mengine na
Mwenyekiti wa Bunge kumsihi mbunge huyo bado aliendelea kuzungumza na
kusimama ikiwa ni kuonesha dharau kwa mamlaka ya Spika na shughuli za
Bunge kinyume na kifungu namba 24 (d) na (e) cha Sheria ya Kinga na Haki
za Bunge.
Barua
hiyo ilieleza kuwa kutokana na vitendo hivyo vinavyokiuka Sheria ya
Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, Sura namba 296 na Kanuni za Bunge,
wabunge hao walionywa kuwa endapo wasingefika mbele ya kamati hiyo jana
hatua za kisheria zingechukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa kifungu cha 15
na 31 (1)(a) na sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini