WALIMU
wa shule ya msingi Kianda wameanza mgomo wa siku mbili wa kutofundisha
shuleni hapo huku wakilaani kitendo cha Ofisa Elimu (Shule za Msingi) wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Peter Fusi
kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao akiwa darasani mbele ya
wanafunzi wake.
Makamu
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Flora Kipesha alisema wameitisha mgomo huo
wa siku mbili kupinga kitendo cha Fusi kumshambulia na kumpiga makofi
mwalimu mwenzao Jacob Msengezi (25) ambaye anafundisha somo la Hisabati
Darasa la Saba shuleni hapo.
“Licha
ya kulaani vikali kitendo hiki cha udhalilishaji alichofanyiwa mwalimu
mwenzetu na Ofisa Elimu (DEO) wetu (Peter Fusi) kumcharaza makofi mbele
ya wanafunzi wake akiwa darasani ….Ametudhalilisha sote yaani hata
hamasa ya kufundisha imetoweka …..
“Sasa
hatutaingia darasani kufundisha kwa siku mbili tukimshinikiza
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga (Adam
Missana) achukue hatua dhidi ya ofisa huyo wa elimu ……yaani
tunadhalilishwa hivi mbele ya wanafunzi wetu wenyewe wakati kazi hii
tumeisomea na tuna vyeti halali ….Tukiwa na sifa stahiki za taaluma ya
ualimu,” alieleza Kipesha.
Akifafanua,
alisema walimu hawataingia kufundisha kwa siku hizo mbili na watakuwa
ofisini wakiandaa mitihani huku wanafunzi wakiendelea kuhudhuria shuleni
hapo kama kawaida.
Mwalimu Msengezi alisema tukio hilo lilitokea Jumatano saa tatu asubuhi
shuleni hapo baada ya ofisa elimu huyo kufanya ziara ya kikazi.
“Nilikuwa na kipindi cha somo la hesabu kuanzia saa mbili hadi saa 2.40 asubuhi kwa kuwa mwalimu wa somo la Kiingereza alikuwa ‘busy’ niliamua kubakia darasani humo nikisahihisha madaftari ya wanafunzi wangu, ndipo nikamwona akiwa eneo la shule, hivyo nikaamua kwenda ofisini kujiandaa na ukaguzi,” alisema.
Aliongeza kuwa, “Wakati nikiwa ofisini aliingia chumba cha darasa la saba na kukuta wanafunzi wakiwa pekee yao, ndipo alipoamuru aitwe mwalimu aliyekuwa akifundisha darasa hilo.
“Nilikwenda darasani na kukutana naye, nilimweleza ilivyokuwa, basi akaniuliza kwani sasa ni saa ngapi?
"Nilipomjibu kuwa ni saa tatu asubuhi alighadhabika na kunipiga makofi. Nilipohisi anajiandaa kuniadhibu zaidi nilitimua mbio na kutoka darasani,” alisema mwalimu huyo.
Aliongeza kuwa tayari ameshafikisha malalamiko yake kwa Katibu wa Chama cha Walimu nchini (CWT) Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Vicent Ndewele kwa hatua zaidi.
Ndewele amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kuwa chama hicho kitatoa msimamo wake kwa vyombo vya habari.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini