Shirika
la Umeme Tanzania Nchini (TANESCO) limewataka wateja wake kuhakikisha
wanaunganishiwa umeme na mafundi au wakandarasi waliosajiliwa na shirika
hilo ili kupunguza ajali za moto.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja wa Afya na Usalama kazini
wa TANESCO, Mhandisi Majige Mabulla alipokua akiongea na waandishi wa
habari juu ya vyanzo vya ajali za moto vinavyosababishwa na umeme.
Mhandisi
Mabulla alisema kuwa matukio ya moto yanayosababishwa na umeme hutokea
kutokana na kuzalishwa kwa joto kali ndani ya nyaya kunakosababishwa na
umeme kuwa mkubwa kuliko uwezo, kulegea kwa maungio ya nyaya pamoja na
radi au nyaya za umeme kuangukia juu ya paa la nyumba.
Kwa
mujibu wa Mhandisi Mabulla aliongeza kuwa ajali za moto
zinazosababishwa na umeme huanza kama unavyoanza moto wa kiberiti au
viwashio vinginevyo vya moto na husambaa haraka kwa kutegemea na aina ya
vitu vilivyopo kwenye eneo husika kwa kuwa baadhi ya vitu hushika moto
haraka na kuenea kwa kasi.
“Ajali
za moto zinazosababishwa na umeme ni ngumu kutokea kama umeme utasukwa
na mtaalam aliyebobea kwenye fani hiyo, TANESCO tunatoa wito kwa wateja
wetu kuhakikisha wanafungiwa umeme na fundi au mkandarasi aliyesajiliwa
na kampuni yetu,”alisema Mabulla.
Pia
Mhandisi Mabulla alisema ili kuepukana na ajali za moto zinazotokana na
hitilafu za umeme wateja wanapaswa ;kuepuka kupitisha nyaya za umeme
juu ya paa za nyumba, kutokuunganisha umeme kutoka nyumba moja kwenda
nyingine bila kupata maelekeza kutoka TANESCO.
Aidha
Mhandisi Mabula alisema wateja pia wanapaswa kuhakikisha mfumo wa umeme
unapitiwa upya kila baada ya miaka mitano pamoja na kuwa makini katika
utumiaji wa vifaa vinavyotumia umeme kama vile pasi, hita za umeme
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini