Sherehe za Mei Mosi : Rais Magufuli Ashusha Kodi ya Mapato Ya Mshahara (PAYE) Kutoka Asilimia 11 Hadi 9 | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Sunday, May 1, 2016

Sherehe za Mei Mosi : Rais Magufuli Ashusha Kodi ya Mapato Ya Mshahara (PAYE) Kutoka Asilimia 11 Hadi 9


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli  ametangaza kushusha kodi ya mapato ya Mshahara ( Pay as you Earn -PAYE  )  kutoka asilimia 11 iliyopo sasa hadi asilimia 9.
Rais amesema ameamua kuchukua umamuzi huo ili kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni ya kuwapunguzia mizigo wafanyakazi kwa kuwaongezea mishahara na kuwapunguzia kodi ya mapato ya mishahara.

Kuhusu kuwaongezea mishahara, Rais Magufuli ameomba wafanyakazi wamvumilie kwa kuwa hivi sasa yuko kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuziba mianya yote ya Rushwa.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewataka waajiri wote nchini kuwapa wafanyakazi wao mikataba ya ajira na kupeleka makato yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii bila kukosa
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin