Kwa
mara nyingine tena Tanzania inashiriki katika onesho la kimataifa la
Utalii la INDABA yanayofanyika huko Afrika Kusini maonesho hayo
yaliyoanza tarehe 7 Mei na yanatarajiwa kumalizika tarehe 9 Mei, 2016
leo jijini Durdan, Bodi ya Utalii (TTB) ndio waratibu wa onesho kwa
upande wa Tanzania. Katika onesho hili TTB inashirki pamoja na taasisi
za TANAPA na Mamlaka na Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na makampuni
mbalimbali binafsi Zaidi ya 30 ya sekta ya Utalii .
Katika
siku yake ya kwanza Banda la Tanzania limetembelewa na wadau wengi
wakiwemo watalii, waandishi wa habari za utalii, mawakala wa Utalii nk.
Miongoni mwa watu mashuhuri waliotembelea Banda la Tanzania ni Mwandishi
maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la
Marekani Bwana Richard Quest ambaye alifurahishwa na vivutio vua utalii
nchini Tanzania mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Maofisa wa Bodi
ya Utalii Tanzania TTB.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini