MKUU
wa Mkoa wa Dares Salaam, Paul Makonda amewasainisha mkataba wakuu wote
wa idara kusimamia na kuhakikisha hakuna mtumishi hewa atakayebainika
kwenye idara zao.
Katika
utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilotoa Machi 15 mwaka huu
kwa wakuu wa mikoa kufuatilia na kubaini watumishi hewa, Mkoa wa Dar es
Salaam umebainika kuwa na watumishi hewa 209 walioisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni mbili.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Makonda alisema hayupo tayari kuendelea kuona watumishi hewa wanaendelea kuwapo.
Alisema
ni jukumu la kila mkuu wa idara kuhakikisha anasimamia eneo lake.
Makonda alisema mkataba utaanza kazi rasmi baada ya siku saba.
Alisema
baada ya hapo, atakayebainika kuwa na mtumishi hewa, atawajibika katika
kulipa gharama zote za hasara alizoingiza kwa malipo yatakayofanyika.
“Nataka
ndani ya siku saba hizi mpitie upya, mhakiki watumishi wenu baada ya
hapo sitataka kusikia sababu yoyote lazima tufanye kazi kila mmoja kwa
nafasi yake na msisubiri kila kitu msimamiwe,” alisema Makonda.
Pia aliwataka wakuu hao kuhakikisha kila mwisho wa wiki wanampelekea taarifa ya kila idara jinsi watakavyofanya kazi.
Wakuu
wa Idara mbalimbali wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wakisaini
mkataba wa kutafuta watumishi hewa katika manispaa zao jijini Dar es
Salaam, na atakaye shindwa kuwafichua baadae wakija kujulikana
atawajibishwa yeye.
Wakuu
wa Idara mbalimbali wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wakiapa kiapo
cha mkataba wa kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jijini la Dar
es Salaam jana walipo apishwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini