GPA ilibadilishwa kwa maoni ya wadau- Ndalichako | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News

Thursday, May 12, 2016

GPA ilibadilishwa kwa maoni ya wadau- Ndalichako

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Joyce Ndalichako amesema mfumo uliotumika kusahihisha matokeo ya sekondari hapa nchini ulikubalika baada ya maonii ya wadau wa elimu kuridhika kwamba ungeleta tija.
Dkt. Ndalichako ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Chadema Susan Lyimo aliyetaka kujua ni kwa nini serikali ilibadilisha mfumo wa kusahihisha kutoka 'Division' kwenda 'GPA' baada ya kuona haufanyi vizuri ni utafiti upi uliwafanya kubadili tena kutoka 'JPA' kwenda 'Division' .
Waziri Ndalichako akijibu swali hilo amesema utaratibu wa kubadilisha mfumo huo ulitokana na maoni ya wadau na baada ya kulalamikiwa sana na wadau wa elimu kwamba GPA kwa upande wa shule za sekondari unaleta mkanganyiko mkubwa ikabidi serikali iubadili.
Aidha Waziri Ndalichako amewataka wananchi kujenga tabia ya kutoa maoni yao inapotokea hali ya kubadilisha mifumo mbalimbali ya serikali kwani serikali hutoa nafasi hiyo ili baadaye kuepuka malalamiko ambayo husababisha kuyumbisha mpango husika.

COMMENTS

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin