Getrude Clement mwenye umri wa miaka 16 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu anayesoma shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza, leo amepata nafasi ya kufika bungeni Dodoma baada ya kupewa mwaliko wa Serikali
Hivi karibuni Getrude alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika New York Marekani ambapo leo Bungeni amewahimiza Watanzania kutunza mazingira na kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali na wataalamu wa mazingira ili kuyatunza mazingira wanamoishi.
Getrude
amesema kuwa amefarijika kwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania na dunia
kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi ambapo mataifa 175 yalikutana
kusaini makubaliano ya Paris.
Katika
kuwahimiza vijana kujenga tabia ya kutunza mazingira, Getrude amewaasa
vijana hasa wanafunzi kusimamia suala la utunzaji wa mazingira wakiwa
shuleni kwa kwa kujiunga na klabu mbalimbali ambapo yeye amejiunga na
klabu ya “Mali Hai” iliyopo shuleni anaposoma.
Kwa
upande wa Watanzania kwa ujumla kwenye utunzaji wa mazingira, Getrude
amesema kuwa ni vema wajifunze kutoka mataifa mengine yanavyosimamia
utunzaji wa mazingira hasa matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mwanafunzi
huyo amekaribishwa na kutambulishwa kwa wabunge leo mjini Dodoma kwa
heshima ya kuliwakilisha vema taifa wakati wa utiaji saini makubaliano
ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo Katibu Mkuu
wa Umoja wa mataifa Ban Ki moon alimkaribisha Getrude kwa viongozi hao
na kusema “Ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni
mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za
vijana”.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini