Gazeti la Raia Tanzania Toleo Na.0615 la Tarehe 15 Aprili, 2016 liliandika taarifa yenye kichwa cha habari “Mbunge apewa mgodi hifadhini” huku likieleza kuwa Mbunge wa Meatu, Salum Khamis Salum (CCM), ametumia ushawishi alionao kisiasa kufanikisha upatikanaji wa leseni ya kuchimba shaba katika eneo la Gururum lililomo ndani ya Hifadhi ya Mwiba, Meatu mkoani Simiyu.
Gazeti
hilo lilieleza kuwa leseni hiyo ilitolewa na Ofisa Madini Kanda ya
Ziwa, Mhandisi Juma Sementa, yenye uhai wa miaka Saba na kwamba
upatikanaji wa leseni hiyo haujawaridhisha wadau kadhaa wa ardhi na
mazingira kwani mbali na sheria ya kuzuia uchimbaji madini ndani ya
maeneo ya hifadhi nchini, wadau wengine hawakuhusishwa katika
upatikanaji wake.
Wizara
inapenda kutoa taarifa kuwa, wilayani Meatu kuna hifadhi ya Maswa
(Maswa Game Reserve) na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori katika eneo la
Makao (JUHIWAPOMA) ambapo Jumuiya hiyo ilipitisha Mpango wa Kanda za
Matumizi ya Rasilimali kwa mwaka 2015-2017 na kutenga eneo la Gururum
lenye ukubwa wa kilomita 16.5 sawa na asilimia 2 ya eneo lote, kama
kanda ya uchimbaji madini baada ya madini ya shaba kugundulika katika
eneo hilo.
Katika
eneo hilo la Gururum mpaka sasa jumla ya viwanja 82 vya uchimbaji mdogo
wa madini (PML) vimetolewa ambapo kwa sasa hakuna shughuli zozote za
uchimbaji zinazoendelea hadi tathmini ya uharibifu wa mazingira (EIA)
itakapokamilika ambayo ipo katika hatua ya uwasilishwaji.
Hivyo
tunautaarifu Umma kuwa mpaka sasa hakuna mgodi katika hifadhi ya Mwiba
na kwamba leseni za uchimbaji mdogo wa madini zimetolewa katika eneo
lililorusiwa tu kwa ridhaa ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori katika
eneo la Makao (JUHIWAPOMA).
Tunawaasa
waandishi wa habari kuhakiki taarifa wanazotoa katika vyombo vya habari
kwa kuwasiliana na wahusika wanaotajwa katika habari husika ili kuepuka
kutoa taarifa potofu kwa Umma.
IMETOLEWA NA WIZARA YA NISHATI NA MADINI
18 APRILI, 2016
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini