WAZIRI wa Fedha na Mipango Mhe. Dakta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini DODOMA, jana tarehe 30, Aprili, 2016, kwamba serikali inaendelea kuhakiki madeni ya walimu yaliyowasilishwa kwaajili ya malipo baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu kwenye baadhi ya madai hayo
Alisema
kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016, serikali ilipokea
madai yenye jumla ya shilingi Bilioni 29 na Milioni 800 na imelipa
20.125bn, huku madai mengine yakizuiwa baada ya kubainika hayakuwa
halali.
Alitolea
mfano wa mtumishi mmoja aliyewasilisha madai ya shilingi 600m badala ya
shilingi laki 6, huku madai mengine yaliyolipwa miaka ya nyuma
yakiwasilishwa kama madeni mapya
Dakta
Mpango alisema kuwa serikali inathamini mchango wa walimu katika
maendeleo ya sekta ya elimu nchini na kwamba itaendelea kulipa madai yao
na watumishi wengine wa umma baada ya kuyachambua, kuyahakiki na
kujiridhisha kuwa ni halali.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini