Makamu Wa Rais Mhe. Samia Azindua Mbio Za Mwenge Wa Uhuru Mkoani Morogoro Leo. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Monday, April 18, 2016

Makamu Wa Rais Mhe. Samia Azindua Mbio Za Mwenge Wa Uhuru Mkoani Morogoro Leo.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro leo.

Katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais alimnukuu Baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere akisema kuwa nia ya Mwenge wa Uhuru tangu mwanzo ni kumulika mipaka ya nchi yetu dhidi ya maadui, kuleta matumaini pale ambapo hakuna matumaini, kuondoa chuki pale ambapo kuna chuki na kuleta heshima pale ambapo kuna dharau.

Alisema nia hiyo ya kuwepo kwa Mwenge wa Uhuru kama alivyomnukuu Baba wa Taifa, inaendana na dhana ya kutumbua majipu katika Serikali ya awamu ya tano. Alisema utumbuaji majipu unalenga kuleta matumaini kwa wananchi ambao wamekata tamaa na kuleta heshima kwa wananchi waliodharauliwa.

“Kaulimbiu ya mbio ya za mwenge mwaka huu ni hii: Vijana ni nguvu kazi ya taifa, washirikishwe na wawezeshwe,”alisema Makamu wa Rais na kuongeza kuwa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa hawajatumika ipasavyo kutokana na sababu mbalimbali.

Alizitaja baadhi ya sababu au changamoto zinazowakabili vijana nchini kuwa ni ukosefu wa ajira, uwezo mdogo wa kuajiri kwenye soko la ajira, ukosefu wa mitaji rafiki kwa vijana, maeneo ya kufanyia kazi pamoja na mitazamo hasi kwa baadhi ya vijana kwa kuchagua kazi.

Makamu wa Rais pia amewataadharisha vijana kutokana na ongezeko kubwa la maambukizi ya ukimwi na matumizi ya madawa ya kulevya. 
Amesema vijana wenye umri kati ya miaka 16-24 ndiyo wanaongoza kwa kuathiriwa na maambukizi ya ukimwi.
 Amesema athari za ukimwi na madawa ya kulevya kwa vijana ni kubwa lakini pia zinaongeza mzigo kwa jamii na serikali katika kuwatibu, kuwahudumia na kuongezeka kwa vifo.

Kwa upande wake, Waziri Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, amemtambulisha George Jackson Kijimba kuwa ndiye kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu akisaidiana na wakimbiza mwenge  wengine watano.
 Alisema sherehe za kuhitimisha mbio hizo za mwenge wa uhuru zitafanyika mkoani Simiyu tarehe 14 Oktoba mwaka huu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Taifa kwenye Sherehe za uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru kitaifa zilizofanyika leo april 18, 2016 katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin