NMB imeanza kupita kila kona kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara kuhusu uwekezaji wa fedha kupitia BOND “Hati fungani”.
Hati Fungani ni namna moja wapo ya kumpa mwananchi njia mbadala ya kuwekeza pesa zake na kuachana na “vibubu”.
Hati Fungani ni namna moja wapo ya kumpa mwananchi njia mbadala ya kuwekeza pesa zake na kuachana na “vibubu”.
Akiongea
na waandishi wa habari, Meneja Mawasiliano Mwandamizi wa NMB Bi.
Joseline Kamuhanda alisema Hati Fungani ni njia moja wapo ya kuwasaidia
wananchi kuachana na tabia ya kuweka pesa zao ndani bila faida yoyote.
“Hati
Fungani inampa mwananchi njia mbadala ya uwekezaji wa pesa, fedha
utayoiwekeza itakupa faida zaidi kulingana na kiasi cha hati fungani
zilizonunuliwa.” alisema.
Ili
kuweza kuwekeza pesa zako kupitia hati fungani unahitaji kuwa na
Central Depository System (CDS account) ambayo inatolewa na Soko la Hisa
la Dar es Salaam. Namba hii hutunza kumbukumbu za mteja katika Soko la
Hisa na pia hutumika katika kununua na kuuza hisa.
Meneja
wa mahusiano ya wawekezaji Bi. Anna Mwasha, akizungumza na waandishi wa
habari alisema uwekezaji kupitia hati fungani utawanufaisha wananchi
wote ambao licha ya kutumia nguvu na rasilimali nyingi, hawapati faida
wanayostahili kutokana na tabia ya kuwekeza pesa zao kwenye vitegauchumi
visivyo na faida ya uhakika.
“Ni
kitu kizuri kwa kuwa ukiwekeza kwenye hati fungani, hata utapokuwa
unataka pesa yako kabla ya muda wa ukomavu, unaweza kuuza hati fungani
hiyo kwenye Soko la Hisa na badala yake, mwananchi mwingine ataendelea
kupokea riba mpaka muda wa ukomavu wa hati fungani, hivyo ni kitu
ambacho ni kizuri kwa kila mtu”. Alisema Meneja wa mahusiano ya wawekezaji
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini